Wajibu wa Mfanyakazi

Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano via Tanzania Mwalimu Julius K. Nyerere kwenye Mkutano wa Kwanza wa NUTA, Dar es Salaam, Julai 34, 1965.

Ndugu Mwenyekiti, Ndugu Wajumbe, na Waheshimiwa wageni wetu,

Leo ni aiku kubwa sana, na mkutano huu una kazi kubwa ya kufanya, Mkutano huu lazima ufikirie jinsi gani chama hiki cha NUTA kilivyochukua madaraka yake mapya kwa watenda kazi wa nchi hii, na jinsi gani watenda kazi nao, kwa kutumia NUTA, ivalivyotimiza wajibu wao kwa taifa letu.

Mkutano huu lazima ufikirie vile vile kazi za baadaye, na kuwafafanulia viongozi wa NUTA, wa TANU na wa Serikali mambo yaliyo muhimu kwa wana-chama wa NUTA. Na jambo lililo muhimu zaidi kwa mkutano huu ni mambo gani wanaehama wenyewe wa NUTA wako tayari kuya-timiza, kwa ajili ya kuendeleza uchumi na hali ya Tanzania kwa sababu ya wajibu huo mkubwa, ni haki kwamba mkutano huu umepata heshima ya kuhudhuriwa na wageni kutoka nchi nyingi.